Waziri wa elimu, sayansi, teknolojia na ufundi Profesa Joyce Ndalichako
ameagiza kusimamishwa kazi kwa Mkuu wa kitengo cha Manunuzi wa Chuo
Kikuu Cha Afya Muhimbili (MUHAS) kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha.
Akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kutembelea chuo hiko, Prof. Ndalichako amesema wamegundua kuwa mnunuzi huyo alikuwa akifanya manunuzi kwa matumizi mabaya ya fedha za umma na sio wa kutenda haki.
Prof. Ndalichako ameendelea kuelezea kuwa kitengo cha manunuzi kinatakiwa kishindanishe watu tofauti, na yeye alikuwa akitumia kampuni 3 zenye majina tofauti ambazo zimekuja kugundulika ni zake.

No comments:
Post a Comment