PICHA ZA MAZOEZI YA YANGA KUJIANDAA NA MECHI NA AZAM FC - TANZA MEDIA ONLINE

Wednesday, 24 January 2018

PICHA ZA MAZOEZI YA YANGA KUJIANDAA NA MECHI NA AZAM FC


Mabeki wa wa timu hiyo Andrew Vicent ‘Dante’, aliyeruka juu na Hajji Mwinyi,wakipokonyana mpira.

KIKOSI cha Yanga leo kimeendelea kujifua kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam ikiwa ni moja ya hatua ya kujiandaa na mchezo wao wa Ligi Kuu Bara, dhidi ya Azam FC utakaochezwa Jumamosi ijayo kwenye Uwanja wa Azam Complex uliyopo Chamazi nje kidogo ya jiji la Dar.

Kiungo wa timu hiyo Papy Tshishimbi Kabamba akipambana na mmoja wa viungo chipukizi wa timu hiyo Maka Edward.

Wakati huo Yanga ambao ni mabingwa wa tetezi wa kobe hilo tayari wameingia kambinitanguja jana jioni ili kuwaweka wachezaji wao kwenye hali sawa kufuatia mchezo huo mgumu kwao.


Nahodha wa timu hiyo Nadir Haroub ‘Cannavaro’, akipambana na mmoja wa mabeki wa timu hiyo,Juma Abdul.

Mawinga wa Yanga Geofrey Mwashiuya na Emmanuel Martin wakigombea mpira wakati wa mazoezi hayo.
Wachezaji wa Yanga wakijinoa kwenye mazoezi hayo.


No comments:

Post a Comment