JESHI
la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam limeeleza kuwa suala la kamata
kamata ya watu waliovaa mavazi ambayo ni kinyume na maadili haliko
chini ya jeshi hilo na badala yake wao husimamia sheria na kulinda
maisha ya watu na mali.
“Suala la mavazi si la
Jeshi la polisi. Ukitaka mimi nitoe ufafanuzi wa mavazi, uniulize habari
zinzohusiana na unifomu za polisi. hizo niko vizuri,” amesema Kamanda Mambosasa.
Hayo yamesemwa leo na Kamanda wa Polisi
Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lazaro Mambosasa alipozungumza kwenye
kipindi cha ‘Morning Tumpet’ kinachorushwa na runinga ya Azam Two na
kueleza kuwa zipo taasisi na mamlaka nyingine zinazohusika na suala la
usimamizi wa maadili, utamadunu pamoja na mavazi.
Kamanda Mambosasa ameeleza kuwa Dhima
ya Jeshi la Polisi ni kulinda usalama wa watu pamoja na mali zao na pia
kusimamisa sheria zilizowekwa.
“Dhima ya Jeshi la Polisi ni kusimamia sheria, kulinda maisha ya watu na mali. Suala la mavazi, zipo taasisi nyingine,” amesema Kamanda Mambosasa.
Jambo hili lilizua taharuki kubwa,
baada ya kuchapishwa habari inayoeleza kuwa watu waliovaa vimini na
kunyoa viduku wamekamatwa na Polisi. Kichwa cha habari hiyo kiliandika.
Hata hivyo, Kamanda Mambosasa, jana
jumatano Januari 17, 2018 akiongea na waandishi wa habari, alikanusha
habari hizo na kueleza kuwa ni za uzushi, huku akiutaka uongozi wa
gazeti la Nipashe kuomba radhi kwa usumbufu liliousababisha.
No comments:
Post a Comment