Maalim Seif Amtembelea Kingunge Hospitali - TANZA MEDIA ONLINE

Thursday, 18 January 2018

Maalim Seif Amtembelea Kingunge Hospitali


Maalim Seif Amtembelea Kingunge Hospitali Kumjulia Hali



January 18, 2018 Katibu Mkuu wa CUF, Maalim Seif Sharif Hamad amemtembelea Mwanasiasa mkongwe nchini Kingunge Ngombale Mwiru aliyelazwa katika wodi ya Mwaisela, hospitali ya Taifa ya Muhimbili.
Maalim Seif amempa pole ya msiba wa mke wake Peras Kingunge, namnukuu Maalim “Tuwe na subira na msiba uliotufika, najua imekuumiza zaid wewe ila ndo ubinadamu sote tunaenda hukohuko, mama katangulia na sisi tunafuata,”

Mzee Kingunge aliruhusiwa kutoka hospitalini hapo Januari 10 ili kwenda kushiriki mazishi ya mkewe, Peras Ngombare Mwiru yaliyofanyika Alhamisi katika makaburi ya Kinondoni jijini Dar es salam.

Mzee Kingunge alilazwa hospitalini hapo baada ya kushambuliwa na mbwa nyumbani kwake eneo la Victoria jijini Dar es salam hivi karibuni.

No comments:

Post a Comment