September 6 2017 Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam
liliamchia kwa dhamana, mwenyekiti wa chama cha ukombozi wa umma
‘CHAUMMA’ Hashim Rungwe baada ya kumshikilia kwa siku 8 kwa kile
kilichodaiwa kuhusika katika utapeli wa Dola za Kimarekani 30,800 ambazo
ni sawa na Tsh Milioni 73 kwa nyakati tofauti akiwa kama Wakili
anayeendesha biashara kati ya raia wa Uturuki Ally Riza Bilgen na
Kampuni ya Les Tropiques Group Mining SPRL Limited.
Inaelezwa kuwa raia huyo wa Uturuki alikuja Tanzania kwa lengo la
kununua korosho tani 15 na kuandikishana mkataba wa malipo ya Dola
72,000 kama gharama za bidhaa hiyo na usafirishaji lakini tangu
wamesainishana mkataba huo November 2016, hakuna kilichofanyika na
malipo hayo ya awali yalifanywa kwenye akaunti ya Rungwe katika Bank ya
CRDB.
Angalia VIDEO Akielezea
No comments:
Post a Comment