Hussein Bashe: Hakuna Mwenye Uhakika na Maisha Yake - TANZA MEDIA ONLINE

Saturday 9 September 2017

Hussein Bashe: Hakuna Mwenye Uhakika na Maisha Yake




                                                      Hussein Bashe.

MBUNGE wa Nzega Mjini, Hussein Bashe
amemtaka Spika wa Bunge, Job Ndugai kuiagiza Kamati ya Bunge ya Ulinzi
na Usalama kukaa na vyombo vya usalama ili kujadili hali ya usalama
nchini ilivyo kwa sasa kufuatia kupigwa risasi kwa Mbunge wa Singida
Mashariki, Tundu Lissu (Chadema).

Bashe aliyasema hayo jana bungeni Mjini Dodoma wakati akielezea tukio la kushambuliwa kwa Lissu.


“Mheshimiwa spika tukio hili
lililotokea ni tukio la kupigwa risasi kwa Tundu Lissu… hoja yangu ni
kwamba, katika nchi yetu kumekuwa na matukio mbalimbali ambayo sisi kama
wawakilishi wa wanachi tunahitaji kupewa taarifa.


“Ben Sanane alipotea hatujasikia kama
wahusika wamekamatwa au la! Msanii ROMA Mkatoliki alitekwa naye
hatujasikia chochote. Waziri Nape Nauye alitolewa bastola hadharani
lakini hatukusikia mhusika huyo akifikishwa katika vyombo vya sheria
wala kusikia kauli yoyote yenye matumaini."


“Jana (juzi), Tundu Lissu alipigwa
risasi tena ndani ya majengo ya nyumba za mawaziri na viongozi, sisi
tunawakilisha Watanzania milioni 50. Matukio haya yanaharibu taswira ya
nchi ya Tanzania, nakuomba Spika, uiagize Kamati ya Ulinzi na Usalama
ikutane na Vyombo vya Ulinzi na Usalama kujadili hali hii ili tuweze
kupata taarifa sahihi kuhusu kinachoendelea, kwa hali inavyoendelea
hakuna mtu mwenye uhakika na maisha yake,”
alisema Bashe.
TIZAMA VIDEO YAKE HII HAPA CHINI

No comments:

Post a Comment