Matokeo ya uchaguzi wa urais nchini Kenya yanaendelea kutangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi (IEBC).
Mgombea
wa urais anahitaji kushinda asilimia 50 na kura moja ili kutangazwa
kuwa mshindi, na pia apate asilimia 25 katika angalau majimbo 24.
Ikiwa
hakuna mgombea atakayepata kura nyingi, basi uchaguzi mpya kati ya
wagombea wawili wanaoongoza utafanyika kabla ya siku 30 kutoka kura ya
kwanza kupigwa kutimia.
Wachanganuzi wameigawana Kenya katika
mikoa kanda tano kikabila: Kikuyu na makundi yanayohusiana nao (asilimia
21), Luhya (asilimia 14), Kalenjin (asilimia 13), Kamba (asilimia 10)
na Luo (asilimia 10).
Uhuru Kenyatta na naibu wake wanarai jamii
zao za Wakikuyu na Wakalenjin, wakati Raila Odinga na naibu wake,
Kalonzo Musyoka (kutoka jamii ya Wakamba), wanatarajia kuungwa mkono na
jamii za Waluo na Kamba.
Odinga pia anatarajia kupata kura nyingi
kutoka jamii ya Waluhya. Musalia Mudavadi, ambaye aliwania urais mwaka
wa 2013, na anatoka jamii ya Waluhya ni muhimu kwenye kampeni ya Raila
Odinga.
- Nani ana nafasi ya kushinda uchaguzi mkuu Kenya 2017?
Kura
kadhaa za maoni zilionyesha ushindani mkali kati ya Kenyatta na Odinga,
na kusababisha watu kuanza kufikiria matukio kadhaa yanayoweza kufuata
baada ya matokeo ya kura kutangazwa.
No comments:
Post a Comment