MBUNGE wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa amepandishwa kizimbani leo Alhamisi katika Mahakama ya Mwanzo Mjini Iringa kwa madai ya kumtusi na kutishia kumuua aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kitwiru, Baraka Kimata.
Mbali na Msigwa pia Diwani wa Viti
Maalum, Selestina Johanes na dereva wa mbunge huyo, Godi Mwaluka
wamepandishwa kizimbani kwa kosa hilo.
Akisoma shtaka hilo Hakimu wa Mahakama
ya Mwanzo, Rehema Mayagilo amesema kuwa mbunge huyo na washtakiwa hao
wawili wanashtakiwa kwa madai ya kumtusi na kutishia kumuua diwani huyo.
Hakimu Mayagilo amesema kuwa Msigwa na
wenzake walitenda kosa hilo jana saa nane mchana katika viunga vya Ofisi
za Halimashauri ya Manispaa ya Iringa.
Baada ya kusomewa shtaka hilo Msigwa na
wenzake wamepata dhamana na kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktober 9 mwaka
huu itakapotajwa tena.
No comments:
Post a Comment