Rais wa Marekani Donald Trump amesema kuwa Korea Kaskazini itakabiliwa kivita iwapo itatoa vitisho kwa Marekani.
Matamshi
yake yanajiri baada ya ripoti ya gazeti la The Washington Post, kudai
maafisa wa ujasusi ambao wanasema kuwa Pyongyang imezalisha kichwa
kidogo cha kinyuklia kinachoweza kutoshea katika makombora yake.
Hii
inamaanisha kwamba Korea Ksakazini inatengeza silaha za kinyuklia
zinazoweza kushambulia Marekani kwa kasi ya juu zaidi ya ilivyodhaniwa.
Umoja wa mataifa hivi majuzi uliidhinisha vikwazo vya kiuchumi dhidi ya taifa hilo.
Baraza
la usalama la umoja wa mataifa lilikubali kuipiga marufuku Korea
Kaskazini kuuza bidhaa zake nje mbali na kupunguza uwekezaji hatua
iliozua hisia kali kutoka kwa Korea Kaskazini ambayo iliionya Marekani.
Mataifa
hayo mawili yamekuwa yakirushiana maneno baada ya Pyongyang kufanyia
majaribio makombora yake ya masafa marefu mnamo mwezi Julai, ikisema
kuwa yana uwezo ya kushambulia Marekani.
Bwana Trump ameambia
wanahabari siku ya Jumanne: Korea Kaskazini isitoe vitisho kwa Marekani.
watakabiliwa kivita kama vile ambavyo ulimwengu haujawahi kuona
No comments:
Post a Comment