- TANZA MEDIA ONLINE

Wednesday, 9 August 2017

 TFF YASEMA USAJILI 2017-18 UI

pic+tff
Usajili wa timu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili kwa msimu wa 2017/18, umekamilika kwa timu 62 tu na timu mbili zimeshindwa kufanya usajili.
Tayari toleo la awali (First Draft) la majina ya timu zote na namna zilivyosajili, tumebandika katika mbao za matangazo za Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Karume Dar es Salaam tangu jana kadhalika nimeunganisha (attach) usajili huo kwenye taarifa hii kwa vyombo vya habari kwa timu zote kwa kufuata alphabeti.
Kubandikwa huko na kusambaza kwenye vyombo vya habari kunalenga kuwapa fursa timu zote kukagua majina ya wachezaji wa kila timu ili kuona kama kuna klabu au mchezaji amefanya udanganyifu wa kusajili wa timu zaidi ya moja, ziweze kuona.
Kama kuna dosari hiyo, TFF imefungua milango ya kupokea pingamizi la usajili wa wachezaji hao kuanzia leo Agosti 8, 2017 hadi Jumatatu Agosti 14, mwaka huu saa 10.00 jioni (16h00).
Kamati ya Katiba, Sheria na Hadhi za Wachezaji inatarajiwa kuwa na kikao ama Agosti 16 au 17, mwaka huu kupitia mapingamizi hayo pamoja na usajili wa timu za Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara. Usajili wa timu za Daraja la Kwanza na Pili, utapitiwa baadaye mwezi huu.
Timu hizo 62 kati ya 64 zimefanya usajili na kuingiza majina ya wachezaji, viongozi wa benchi la ufundi kwenye mfumo wa mtandao wa TMS – Transfer Matching System. 
Timu ambazo zimeshindwa kufanya hivyo yaani usajili kwa mfumo wa TMS ni za Ligi Daraja la Pili (SDL) ambazo ni Pepsi ya Arusha na Bulyanhulu ya Shinyanga.
Na kwa msingi huo, timu hizo za Pepsi na Bulyanhulu zimejitoa kushiriki ligi kwa msimu wa 2017/18 na zinashushwa daraja hadi ligi ya wilaya kuanza upya kutafuta nafasi za juu kupanda daraja.
……………………………………………………………………………………….
IMETOLEWA NA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA

No comments:

Post a Comment