Nchi ya Misri imepiga hatua nyingine ya kiteknolojia siku za hivi karibuni baada ya kuzindua mtandao wake mpya unaofanana na Facebook, unaojulikana kama EgyptFace.
Inaelezwa kuwa Waziri wa Mawasiliano nchini humo, Yasser Al-Qadi, alitangaza wiki chache zilizopita kuwa serikali inatarajia kuzindua mtandao wake, jambo ambalo watu wanaamini mtandao huo ulitengenezwa haraka haraka.
Rais wa nchi hiyo ameeleza kuwa wanaamini mtandao huo umeundwa ili kwamba vyombo vya usalala vifuatilie kwa ukaribu watumiaji wake na taarifa zao.
Inaripotiwa kuwa siku za hivi karibuni watu wengi wamefungiwa akaunti zao za mtandao wa Facebook huku wengine wakikamatwa na Jeshi la Polisi kwa tuhuma za uchochezi.
No comments:
Post a Comment