KOCHA wa Simba, Pierre Lecha-ntre ametamka kwamba hakuna chochote
wanachokitaka leo kwa Ruvu Shooting yenye msemaji mwenye mbwembwe,
Massau Bwire zaidi ya pointi tatu. Kocha huyo mfaransa mwenye wasaidizi
wawili amesisitiza kuwa kikosi chake kiko sawa wala hana mchecheto
wowote ingawa rekodi za ushindi zinamzidishia jeuri.
Mchezo huo ambao utapigwa kwenye Uwanja wa Uhuru jijini Dar es
Salaam, unatajwa kuwa ni wa kisasi kutokana na mchezo wa awali
kumalizika kwa Simba kushinda mabao 7-0. Simba iliyopo kileleni na
pointi zake 35, itapambana na Ruvu iliyopo nafasi ya 12 kutokana na
kujikusanyia pointi 14.
Tangu msimu wa 2011/12 na kabla ya mchezo wa leo, timu hizo
zimekutana mara kumi. Msimu wa 2015/16 timu hizo hazikukutana kutokana
na Ruvu Shooting kushuka daraja.
Katika michezo hiyo, Simba imeshinda mara tisa na kutoka sare moja.
Ilivyokuwa Msimu wa mwaka 2011/12, Simba ilishinda 2-0, kisha ikashinda
tena 1-0. Msimu uliofuata Simba ikashinda 2-1, ziliporudiana Simba
ikashinda 3-1. Katika msimu wa 2013/14, matokeo yalikuwa hivi; Ruvu 1-1
Simba, Simba 3-2 Ruvu.
Msimu wa 2014/15 Simba 1-0 Ruvu, Ruvu 0-3 Simba na msimu uliopita
Simba 2-1 Ruvu Shooting, Ruvu 0-1 Simba. Mabao Katika hiyo michezo
ambayo wamekutana kwenye misimu tofauti, jumla ya mabao 32 yamefungwa.
Simba imefunga mabao 26 na Ruvu sita. Wanachokisema makocha Kocha
Mkuu wa Simba, Pierre Lechantre raia wa Ufaransa, kuelekea mchezo huo,
amesema: “Kikubwa tunahitaji pointi tatu za kila mchezo ulio mbele yetu
ili tumalize tukiwa mabingwa.”
Abdulmutik Haji ambaye ni Kocha Mkuu wa Ruvu Shooting, amesema:
“Tunafahamu tunaenda kukutana na timu ya aina gani, nimewaandaa vijana
wangu kwa ajili ya kupata matokeo mazuri ili tuweze kuwa sehemu salama
zaidi.”


No comments:
Post a Comment