MBUNGE wa Iringa Mjini, Mchungaji Peter Msigwa (CHADEMA) na wenzake 12 wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Iringa na kusomewa mashtaka ya tuhuma zinazowakabili.
Msigwa na wenzake wanatuhumiwa kula njama za kuchoma moto nyumba ya Katibu wa Umoja wa Viajana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM) mkoani humo na kubomoa nyumba ya aliyekuwa Diwani wa Kata ya Mwangata aliyehamia CCM, Angelus Lijuja.
Aidha, upande wa mashtaka uliwasilisha kiapo cha pingamizi ya dhamana kwa watuhumiwa hapo lakini Mahakama imetupilia mbali pingamizi hilo na watuhumiwa wamepewa dhamana.
No comments:
Post a Comment