Jeneza lenye mwili wa Marehemu Mama Peras Ngombale Mwiru ukiwasili nyumbani.
Jeneza
lenye mwili wa Marehemu Mama Peras Ngombale Mwiru, Mke wa Mmoja waasisi
wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Mzee Kingunge Ngomale Mwiru ukiwasili
nyumbani tayari kwa ibada maalum ya maombolezo, iliyofanyika jioni ya
jana. Marehemu Mama Peras Ngombale Mwiru anatarajiwa kuzikwa leo jioni
kwenye makaburi ya Kinondoni, jijini Dar es salaam.
Rais
Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete akimfariji Mzee Kingunge Ngomale Mwiru kwa
kufiwa na Mkewe, Mama Peras Ngombale Mwiru, alipofika Nyumbani kwale
Victoria, jijini Dar es salaam jana. Katikati ni Mzee Ally Mtopa.
Rais
Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete akisalimiana na Mwenyekiti wa Chama cha
Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe wakati walipokutana
kwenye Msiba wa Mama Peras Ngombale Mwiru, Mke wa Mmoja waasisi wa Chama
cha Mapinduzi (CCM), Mzee Kingunge Ngomale Mwiru, nyumbani kwake
Victoria, jijini Dar es salaam jana.
Waziri
Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba akimfariji Mzee Kingunge Ngomale
Mwiru kwa kufiwa na Mkewe, Mama Peras Ngombale Mwiru, alipofika Nyumbani
kwale Victoria, jijini Dar.
Naibu
Katibu Mkuu wa CCM Bara, Rodrick Mpogolo akiwa ameambatana na viongozi
Wengine wa Chama hicho waliofika nyumbani wa Mzee Kingunge Ngomale Mwiru
kumfariji kwa kufiwa na Mkewe, Mama Peras Ngombale Mwiru.
Viongozi mbalimbali wakiongea na Mzee Kingunge.
Sehemu ya wanafamilia wakiwa ni nwenye majonzi kwa kuondokewa na mpendwa wao.
Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Kikwete na Viongozi mbalimbali wa vyama na serikali wamefika nyumbani kwa Mzee
Kingunge Ngomale Mwiru, nyumbani kwake Victoria, jijini Dar es salaam
kumfariji jana baada ya kufiwa na mke wake Peras Ngombale hivi
karibuni na anatarajiwa kuzikwa leo jioni kwenye makaburi ya Kinondoni,
jijini Dar es salaam.
PICHA NA MICHUZI
No comments:
Post a Comment