Polisi nchini
Denmark wanachunguza kisa cha wizi wa chupa ya mvinyo inayodaiwa kwa
ghali zaidi duniani ya thamani ya dola milioni 1.3.
Chupa hiyo
iliyotengenezwa kutoka kwa dhahabu na fedha na kifuniko cha almasi
ilikopeshwa baa moja huko Copenhagen ambayo ilikuwa imekusanya chupa za
mvinyo kwa maonyesho.
Mmiliki wa baa hiyo Brian Ingberg alisema chupa ilikuwa imetumiwa kwenye kipindi kinachofahamika kama House of Cards.
Picha za CCTV zinaonya mvamizi akishika chupa hiyo na kutoroka.
Polisi wanasema kuwa haijuikani ikiwa mwzi huyo ambaye alivamia siku ya Jumanne alivunja au alikuwa na ufunguo.
Bw.
Ingberg ambaye ni mmliki wa bar aliiambia runinga ya TV2 kuwa alikuwa
ameikopa chupa hiyo kutoka kwa kampuni moja huyo Latvia.
No comments:
Post a Comment