JESHI la Polisi Kanda Maalumu yaDar es
Salaam, limesema kesi ya Dk Louis Shika hawataendelea nayo kwa kuwa
nyumba tatu za mfanyabiashara maarufu Said Lugumi alizoahidi kuzinunua
zote zipo na hazijapata mnunuzi.
Hayo yamesemwa leo Desemba 6, 2017 na
Kamanda wa Polisi Kanda maalum ya Dar, Lazaro Mambosasa wakati
akizungumza na wanahabari, amesema kesi ya Dkt. Shika haina mashiko
hivyo hawataendelea nayo kwa kuwa nyumba hizo zipo na hajatia hasara
yotote.
Mambosasa amesema Dk Shika alikuwa
akitamba kuwa ana fedha kumbe uwezo wake ni mdogo na kusababisha
kushindwa kulipa asilimia 25 kwa kila nyumba hizo.
‘‘Dk Shika ni wa kumuonea huruma hana
kitu, tulisema tunamchunguza na tutampeleka mahakamani lakini tumeona
kesi yake haina mashiko ndiyo maana tumeamua tusiendelee nayo,” amesema Mambosasa.
Novemba 9, 2017 kampuni ya udalali ya
Yono kwa niaba ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) iliendesha mnada wa
hadhara wa nyumba mbili za Lugumi zilizoko Mbweni JKT na nyingine Upanga
jijini Dar es Salaam ambazo zote Dk Shika alifikia bei ya kuzinunua kwa
Tsh. Bilioni Sh 3.2.
Jeshi la polisi kanda hiyo
lilimshikilia na kumwachia kwa dhamana Dk Shika ambaye alikuwa
akituhumiwa kwa kuharibu mnada baada ya kushindwa kulipa asilimia 25 ya
fedha hizo ambapo nyumba za Mbweni JKT alifika bei kwa Sh. 900 milioni
na nyingine Sh 1.1 bilioni, huku ya Upanga alifika bei ya Sh 1.2
bilioni.
(Stori na Pamela Chilongola, Mwananchi)
No comments:
Post a Comment