Jeshi la Marekani limerusha ndege yake aina ya B-1B bomber katika anga
ya Korea Kusini kama sehemu ya mazoezi ya pamoja ya angani katika hatua
inayoonekana kama onyo kwa Korea Kaskazini.
Mazoezi hayo ya kijeshi yanafanyika wiki moja baada ya Korea Kaskazini
kurusha kombora ililodai kuwa ni la masafa marefu ambalo linaloweza
kushambulia nchini Marekani.
Ndege za kivita za Marekani zapaa Korea
Marekani awali imerusha ndege hizo zenye uwezo wa juu kuonyesha ubabe
baada ya majaribio ya makombora ya Korea Kaskazini au majaribio ya
mabomu ya nyuklia.
Zaidi ya ndege 200 na maelfu ya wanajeshi wanashirikia katika mazoezi hayo ya kijeshi ambayo yatakamilika siku ya Ijumaa.
Pyongynag ambayo mara nyini hukashifu mazoezi ya pamoja ya Marekania na
Korea Kusini, imeyataja mazoezi ya sasa kuwa uchokozi wa vita vya
nyuklia.
Misukosuko imekuwa ikiongezeka tangu lifanyike jaribio la kombora mwezi
uliopita lililosababisha lawama za kimataifa na onyo kutoka Marekani
kuwa Korea Kaskazini itaharibiwa aabisa ikiwa vita vitatokea.
No comments:
Post a Comment