TFF Yakabidhi Ripoti ya Maandalizi ya Mashindano ya Afcon Mwaka 2019 - TANZA MEDIA ONLINE

Thursday, 28 September 2017

TFF Yakabidhi Ripoti ya Maandalizi ya Mashindano ya Afcon Mwaka 2019

Mwakyembe Akabidhiwa Ripoti ya Maandalizi ya Mashindano ya Afcon Mwaka 2019

 

Kuelekea katika mashindano ya Afcon U-17 mwaka 2019 ambapo Tanzania ndiyo wenyeji, Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na michezo Dkt. Harrison Mwakyembe amesema atahakikisha mashindano hayo yanaenda vizuri bila ya kuwa na tatizo lolote.


Dkt. Mwakyembe amesema hayo katika kikao cha ufunguzi wa mashindano hayo yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam na kuahidi kufuatilia kwa ukaribu ukarabati wa viwanja pamoja na timu ili kujihakikishia kuwa hakuna tatizo kwa upande wa maandalizi.

"Uenyeji wa mashindano haya hatuja yapokea kwa gafla hivyo tutahakikisha tunafanya maandalizi mazuri kwa timu yetu na miundombinu ili kuhakikisha nchi yetu ya Tanzania inafanya vizuri katika mashindano hayo", amesema Dkt. Mwakyembe.

Naye Makamu wa Rais wa Kamati ya ufundi ya maendeleo ya shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) ambaye pia ni mwakilishi wa ukanda wa Afrika Mashariki, Leodgar Chilla Tenga amesema anaendelea kuhamasisha zaidi ili kuhakikisha heshima ya Tanzania katika maandalizi inafanikiwa kwa kiwango kikubwa.

"Heshima ya nchi katika soka ni uwezo wa kuandaa mashindano pamoja na kuyafanikisha kwa kiasi kikubwa. CAF wanamatumaini makubwa na Tanzania juu ya uenyeji wa mashindano haya japo kuna mahitaji mengi lakini yanawezekana kufanikishwa", amesema Tenga.

Kwa upande wake,  Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Wallace Karia amesema licha ya maandalizi ya miundombinu lakini watahakikisha wanaiandaa timu vizuri kwani mashindano hayo ni sehemu ya kufuzu kushiriki mashindano ya kombe la dunia la vijana.

No comments:

Post a Comment