Serikali ya Tanzania imejipanga kuongeza vituo 150 nchini kwa ajili ya
kutoa huduma ya uzazi wa dharura ili kuokoa vifo vinavyotokana na uzazi
pingamizi nchini.
Hayo yamebainishwa na Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na
Watoto Mhe. Ummy Mwalimu, katika kikao cha wabunge wa klabu ya uzazi
salama kilichofanyika Mkoani Dodoma.
"Sisi awamu ya tano katika mwaka wetu huu mmoja tutaongeza vituo 150
katika kufanikisha uokoaji huo serikali pia imeandaa fedha kwa ajili ya
kujenga vituo vitano vya kuhifadhia damu salama kwa ajili ya upasuaji wa
akina mama wanaojifungua", amesema Waziri Ummy.
Waziri wa Afya Maendeleo ya Jamii Jinsia Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu.Kwa upande wake Mwenyekiti wa klabu hiyo ambaye pia ni Waziri wa Nchi
Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Uratibu, Bunge, Kazi,Ajira, Vijana na wenye
Ulemavu, Mhe. Jenista Mhagama ametaka usimamizi wa fedha katika vituo
vya Afya katika halmashauri zitumike kwa matumizi yaliyopangwa na wala
isiwe vinginevyo.
Kwa taarifa zaidi msikilize hapa chini Waziri Ummy Mwalimu pamoja na
Waziri Jestina Mhagama wakiongelea suala la kuongeza vituo vya afya ili
kuweza kuokoa vifo vinavyotokana na uzazi
No comments:
Post a Comment