KAMANDA wa Polisi wa Mkoa wa Dodoma,
Gilles Muroto amemtaka dereva wa Mbunge wa Singida Mashariki (Chadema)
Tundu Lissu, ajitokeze ili aweze kutoa maelezo yake kuhusiana na tukio
la kupigwa risasi bosi wake.
Kamanda huyo amesema kwamba sababu ya
kumtafuta dereva huyo aliyemtaja kwa jina la Adam ni kwa sababu alikuwa
pamoja na majeruhi wakati tukio hilo linatokea.
Pia Kamanda huyo alimtaka Katibu Mkuu
wa Chadema Dk Vicent Mashinji kufika kwa RCO mjini Dar es Salaam ama
Dodoma kutokana kauli yake kuwa katika uchunguzi wao wamewabaini
wahusika.
Kamanda Muroto amesema Polisi Mkoani
Dodoma wamekamata magari nane aina ya Nissan Patrol kwa ajili ya
uchunguzi wa tukio la kupigwa kwa risasi kwa mbunge wa Singida Mashariki
(Chadema) Tundu Lissu.
Kamanda Muroto amesema uchunguzi huo unafanywa kwa kushirikiana na Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA).
“Uchunguzi wa awali umeonyesha kuwa
wahalifu walikuwa na silaha ya SMG/SAR kutokana na maganda ya risasi
yaliyokutwa eneo,” amesema
No comments:
Post a Comment