Kauli ya Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige dhidi ya ACACIA - TANZA MEDIA ONLINE

Wednesday 6 September 2017

Kauli ya Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige dhidi ya ACACIA

Kauli ya Mbunge wa Msalala, Ezekiel Maige baada ya ACACIA kutangaza kupunguza Shughuli zake katika mgodi wa Bulyanhulu
 
Nimepata taarifa ya Acacia kupunguza shughuli zake BULYANHULU na hivyo kuleta tiahio la madhara ya kiuchumi kwa wafanyakazi zaidi ya 1,200; wakandarasi zaidi ya 800 na wananchi kaka maelfiu Kakola na maeneo jirani. Hali hii haipaswi kuachwa hivi hivi.

My immediate reaction kwa hali hii ni KUIOMBA SERIKALI IRUHUSU WANANCHI AMBAO NI WACHIMBAJI WADOGO KWA MAISHA YAO YOTE, WAANZE KUCHIMBA REEF 2 na maeneo mengine yenye madini ndani ya leseni ya Acacia pembeni ya mgodi ili maisha yaendelee.

Ni vema pia seriklai ikasimamia kuhakikisha haki za wananchi, hasa wafanyakazi na wakandarasi wenye mikataba zinalindwa wakati huu. Serikali isiwaache wafanyakazi wakafanyiwa anachopenda mwekezaji. Ni muhimu SERIKALI ifanye hivyo ili wajue there are consequences for any action they take.

Nawasihi wananchi wangu (hasa wafanyakazi, wakandarasi na wengine ambao wamepata madhara ya moja kwa moja) tuendelee kuwa watulivu tukiamini Mazungumzo yanayoendelea kati ya SERIKALI na Barrick yatapelekea haki zetu zilizoporwa siku zote kurejeshwa na neema endelevu kupatikana.

Mawasiliano rasmi kati ya ofisi yenu (ya Mbunge) na SERIKALI kuhusu maombi mnayopenda SERIKALI iyafanyie kazi kwa jinsi mambo yanavyokwenda yanafanyika.

No comments:

Post a Comment