KAIMU Katibu Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Alfred Kidao
amesema kuwa ameagizwa na rais wa Shrikisho hilo, Wallace Karia
kumwandikia barua Mtendaji mkuu wa Bodi ya Ligi ili kuwaadhibu viongozi
wa Bodi ya Ligi waliohusika na kupanga ratiba.
Kumekuwa na malalamiko kutokana na Bodi hiyo kupanga ratiba ya ligi
ambapo walishindwa kuzingatia kuwa kuna michezo ya kimataifa ambayo
itahusisha timu za taifa jambo ambalo limesababisha baada tu ya mchezo
mmoja tu, ligi hiyo ikapanguliwa tena.
“Nimeagizwa na rais nimwandikie barua mtendaji mkuu wa bodi ya ligi
ili aweze kuwachukulia hatua viongozi wa bodi hiyo waliohusika na
kupanga ratiba hii pamoja na kwamba walikuwa na kalenda lakini bado
wamekosea,” alisema Kidao.
Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi ni Boniface Wambura ambaye sasa atakuwa na jukumu la kuchukua hatua kwa wasaidizi wake.
No comments:
Post a Comment