Marais wastaafu, Benjamin Mkapa na Jakaya Kikwete wamekutana kwa mara ya kwanza katika jukwaa moja wakiwa nje ya nchi wakihudhuria mkutano unaoratibiwa na Uongozi Institute kwa kushirikiana na Taasisi ya Mbeki.Mkutano huo unaomalizika leo unafanyika Johannesburg Afrika Kusini na kuhudhuriwa na marais kadhaa wastaafu.
Hii ni mara ya kwanza kwa marais hao kushiriki tukio la pamoja wakiwa nje ya nchi tangu Rais Kikwete
aondoke marakani mwaka 2015. Ingawa viongozi hao wamekuwa wakishiriki
katika shughuli mbalimbali za kimataifa lakini hawajawahi kukaa jukwaa
moja wakiwa nje ya nchi.
Marais wengine wastaafu wanaohudhuria mkutano huo ni pamoja na aliyekuwa Rais wa Nigeria, Olusegun Obasanjo na Hassan Sheikh Mohamud aliyekuwa rais wa Somalia.
Picha za video zinazorusha mkutano huo
zimewaonyesha marais hao wakiwa katika jukwaa moja wakipiga picha baada
ya kumaliza majadiliano ya sehemu ya kwanza.
Katika upigaji picha, Rais Kikwete
ameonekana akiwa ameketi mwanzo akiwafuatiwa na rais wa Nigeria,
Obasanjo na kisha kufuatiwa na Mahamud wa Somalia. Rais Mkapa ameketi
nafasi ya nne akifuatiwa na kiongozi mwingine ambaye hakuweza
kutambulika mara moja na mwishoni aliketi Rais Thabo Mbeki ambaye
taasisi yake ndiyo mwenyeji wa mkutano huo.
Mara baada ya kumalizika kwa shughuli
ya upigaji picha, Rais Kikwete alionekana akijadiliana jambo kwa karibu
na Rais Obasanjo na kisha viongozi hao waliteremka kutoka jukwaani.
Wakati akielekea kwenye eneo lake
Kikwete aliwasalimia wageni kadhaa ndani ya mkutano huo na baadaye
alielekea sehemu aliyokuwa amesimama aliyekuwa katibu mkuu kiongozi,
Ombeni Sefue na kuonekana akimsisitizia jambo na kisha akaondoka.
Viongozi hao wamekuwa wakijadiliana
kuhusu masuala ya demokrasia, utawala bora na jinsi ya kuzisaidia nchi
za Afrika kusonga mbele kimaendeleo.
No comments:
Post a Comment