Hatimaye utata uliokuwa umeenea wa
kuwepo kwa ufujaji na matumizi mabaya ya fedha kiasi cha milioni 285.49
zilizokuwa zimechangwa na wadau pamoja na serikali kwa ajili ya rambi
rambi ya vifo vya ajali ya basi la wanafunzi wa shule ya Lucky Vicent
umekwisha baada ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo kukabidhi
milioni 23.27 kwa wazazi wa watoto walionusurika katika ajali hiyo.
Akikabidhi fedha hizo mbele ya
waandishi wa habari ambapo kila mzazi alipata Tsh. Milioni 7.75, Gambo
alisema fedha hizo zilikuwa zimebaki baada ya matumizi ya shughuli za
mazishi kwa watoto 32 walimu wawili na dereva waliokuwa wamekufa katika
ajali hiyo na matumizi mengine yakiwemo ya wazazi waliokuwa nchini
marekani kwa ajili ya kuwauguza watoto wao na kwamba matumizi ya fedha
hizo watapanga wao wenyewe.
Katika hatua nyingine Gambo alisema
Serikali imekubali kutoa wataam wa saikolojia kwa ajili ya kuendelea
kuwasaidia watoto walionusurika katika ajali ya basi la wanafunzi ili
kuwaweka sawa na pia kuwaandaa kufanya mtihani wa darasa la saba
unaowakabili mnamo mwezi Septemba.
Mhe Gambo akisalimiana na mtoto Doreen Mshana.
Aidha Gambo alisema kazi ya kutoa tiba
ya kisaikolojia pia ilishafanyika kwa wanafunzi wa shule ya Lucky
Vicent. Wakizungumza baada ya kukabidhiwa fedha hizo wazazi wa watoto
hao wameishukuru serikali na wafadhili kutoka marekani kwa msaada mkubwa
kwa watoto wao tangu mwanzo hadi sasa.
Aidha wazazi hao walisema pamoja na
watoto wao kuwa nje ya shule kwa zaidi ya miezi mitatu wako tayari
kufanya mtihani na kumaliza elimu ya msingi unaotarajiwa kufanyika mwezi
September.
Kwa mujibu wa Gambo, baada ya kutokea
kwa ajali hiyo mwezi Mei 2017, wadau mbalimbali na serikali walijitolea
na kuchanga fedha na kupatikana zaidi ya milioni 285.49 ambazo nbaada ya
matumizi zilibaki milioni 23.27 ambazo zilikabidhiwa jana.
No comments:
Post a Comment