WATOA mada mashuhuri nchini, Maria
Sarungi Tsehai anatarajiwa kuungana na Lawrence Marsha, Eric Shigongo,
Mzee Shaba na Benjamin Fernandes katika kongamano la kihistoria la Meza
ya Wazalendo litakalofanyika Septemba 2, mwaka huu ndani ya Ukumbi wa
Nkurumah, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
Akizungumza na Risasi Vibes, mratibu wa
kongamano hilo kutoka Taasisi ya Vijana Wazalendo wa Kitanzania,
Tanzania Youth Patriots (TYP), Vian Nchimbi alisema kuwa, siku hiyo
ratiba itaanza rasmi saa 7 mchana hadi saa 11 jioni ambapo mgeni rasmi
anatarajiwa kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais
anayeshu-ghulikia Muungano na Mazingira, January Makamba.
“Tutakuwa pia na mtangazaji maarufu
kutoka Kituo cha Redio cha Sauti ya Amerika (VoA), Shaka Ssali
tunawa-omba wote mje kuwa sehemu ya mjadala mpana ambapo mambo
mbalimbali juu ya Utanzania wetu na dhana nzima ya uzalendo kwa ujumla
yatazung-umzwa.
“Wanafunzi wa sekondari, vyuo vya elimu
ya juu, taasisi mbalimbali na wananchi wote mnakaribishwa kwani
kiingilio ni bure kabisa,” alisema Vian.
Kwa mawasiliano zaidi, unaweza kupiga simu au ujumbe wa SMS au WhatsApp kupitia namba 0769984781. Kongamano hili limedhaminiwa na Clouds Media Group na Global Publishers.
No comments:
Post a Comment