Mbunge Godbless Lema apanda kizimbani leo - TANZA MEDIA ONLINE

Monday 21 August 2017

Mbunge Godbless Lema apanda kizimbani leo

Image result for lema godbless


Mahakama ya Wilaya ya Arusha imeahirisha kumsomea maelezo ya awali ya kesi mbili za uchochezi zinazomkabili Mbunge wa Arusha Mjini Godbless Lema kutokana na upande wa Serikali kudai kwamba Jalada la kesi hiyo bado lipo kwa Mkurugenzi wa Mashtaka.
Wakili wa Serikali Agnes Nyera ameiomba Mahakama kuahirisha shauri hilo kwa kuwa hawataweza kumsomea maelezo ya awali kutokana kutokuwa na Jalada hivyo ameahidi kumsomea wakati ujao.
Hakimu anayesikiliza kesi hiyo Devotha Msofe ameahirisha kesi hadi September 20, 2017 huku akiutaka upande wa mashtaka kuhakikisha wanawasilisha maelezo ya awali Mahakamani hapo

No comments:

Post a Comment