Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Simon Siro (katikati aliyeshika kiuno) akiongea na viongozi wa jeshi lake Tangibovu, Kibiti, wakati wa kuonyesha silaha walizokamata kutoka kwa watu wanaodaiwa kuwa wahalifu.
JESHI la Polisi nchini Tanzania limesema wahalifu 13 wameuawa katika
majibizano ya risasi katika eneo la Tangibovu lililopo katika kijiji cha
Miwaleni, tarafa ya Kibiti mkoani Pwani na kukamata bunduki nane,
pikipiki mbili na begi la nguo.
Jeshi hilo limeendeleza jitihada zake kuhakikisha mkoa wa Pwani na
maeneo yake ya jirani yanakuwa salama na yenye amani kwa kuendelea
kupambambana na wahalifu mbalimbali waliojificha mkoani humo ambao
wamekuwa wakifanya matukio mbalimbali ya kihalifu.
Rais John Pombe Magufuli alipokuwa katika ziara mkoa wa Pwani mwezi
Juni mwaka huu aliwataka wahalifu wote waliopo mkoani humo waache mara
moja kufanya matukio ya kihalifu, ambapo pia Mkuu wa Jeshi la Polisi
(IGP) Simon Sirro aliwataka wahalifu kuacha mara moja uhalifu mkoani
humo na kuwaambia kuwa mkono wa dola utawafikia kama wataendelea.
Mkoani Pwani zaidi wa watu 30 wameuawa na watu wasiojulikana kwa
vipindi tofauti huku jeshi la polisi nalo likifanikisha kuwaua zaidi ya
wahalifu 20 wanaodaiwa kuhusika na matukio mbalimbali yakiwemo
yaliyokuwa yakifanyika mkoani humo na maeneo jiran
No comments:
Post a Comment