Wema: Sijawahi ‘Kummisi’ Kajala, Muna - TANZA MEDIA ONLINE

Friday 11 August 2017

Wema: Sijawahi ‘Kummisi’ Kajala, Muna

 
STAA wa filamu mwenye nyota ya kipekee Bongo, Wema Sepetu amefunguka kwa mara ya kwanza kuwa hajawahi kuwakumbuka (kuwamis) waliokuwa mashoga zake wa damu, Muna Alphonse ‘Muna’ na Kajala Masanja na kudai alishawatoa kwenye akili yake.

 Akizungumza na Star Mix kinachoongozwa na Imelda Mtema , Wema alisema kuna baadhi ya watu ambao hajaonana nao muda mrefu na anawakumbuka kila mara lakini kwa upande wake hajawahi kuwakumbuka rafiki zake hao ambao huko nyuma walikuwa kama kumbikumbi.


“Sitaki kusema dhambi jamani sijawahi kuwamisi hawa watu (Muna na Kajala) kabisa naona kama niliwafuta kwenye kichwa changu maana najikuta kuna watu nawakumbuka lakini hao hapana,” alisema Wema.

chanzo:global publishers

No comments:

Post a Comment