Korea Kaskazini Yaonywa na Baraza la Usalama la UN - TANZA MEDIA ONLINE

Wednesday 30 August 2017

Korea Kaskazini Yaonywa na Baraza la Usalama la UN

 Korea Kaskazini Yaonywa na Baraza la Usalama la UN


Baraza la usalama la Umoja wa Mataifa limelaani kitendo cha Korea Kaskazini cha kurusha kombora kupitia anga ya Japan, huku nchi hiyo ikithibitisha kutekeleza.

Taarifa iliyoandikwa na Marekani, haikutishia kuiwekea vikwazo vipya Korea kaskazini.Lakini Baraza la Usalama limeitaka Korea Kaskazini kusitisha majaribio zaidi na kusitisha mpango wake wa nyuklia.

Wanachama 15 wa Baraza hilo la Usalama wameitaka Korea Kaskazini kuchukua hatua za haraka kupunguza hali ya wasiwasi uliyopo.Majeshi ya Korea Kusini na Marekani yamekuwa yakifanya mazoezi ya pamoja karibu na mpaka wa Korea Kaskazini, jambo ambalo Pyongyang inasema ni mazoezi yenye kulenga uvamizi wa kijeshi

No comments:

Post a Comment