Kesi ya Aveva, ‘Kaburu’ Yapigwa tena kalenda - TANZA MEDIA ONLINE

Wednesday 30 August 2017

Kesi ya Aveva, ‘Kaburu’ Yapigwa tena kalenda

Kesi inayomkabili Rais wa Simba, Evans Aveva na makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’  leo imeendelea katika mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu ambapo upande wa mashtaka umeieleza mahakama hiyo kwamba umekusanya nyaraka za upelelezi na zimepelekwa kwa mtaalamu wa maandishi hivyo hivyo wanasubiri ripoti.

Hayo yamesemwa na Wakili wa Serikali, Estazia Willson mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa wakati kesi hiyo ilipoitishwa kwa ajili ya kutajwa ambapo aliiiomba mahakama iahirishe kesi hiyo hadi Septemba 8 mwaka huu.

Aidha hakimu aliutaka upande wa mashtaka kuharakisha ripoti hiyo ya uchunguzi akisema kwamba watuhumiwa wako rumande hivyo si bora kesi hiyo kuahirishwa kila mara

 Hakimu Nongwa ameahirisha kesi hiyo hadi September 8, 2017.

No comments:

Post a Comment