Kesi ya Aveva, Kaburu TAKUKURU yakiri upelelezi haujakamilika - TANZA MEDIA ONLINE

Wednesday 16 August 2017

Kesi ya Aveva, Kaburu TAKUKURU yakiri upelelezi haujakamilika


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo August 16, 2017 imeitaka TAKUKURU kuhakikisha inafika na taarifa ya uhakika kuhusu upelelezi wa kesi inayowakabili Rais wa Klabu ya Simba, Evans Aveva na Makamu wake, Geofrey Nyange ‘Kaburu’ ifikapo August 30, 2017.
Mwendesha Mashtaka wa TAKUKURU, Leornad Swai amemueleza Hakimu Mkazi Mkuu, Victoria Nongwa kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika ambapo baada ya kueleza hayo, Hakimu Nongwa alimtaka Swai aeleze upelelezi umefikia hatua gani.
Swai alidai kuwa kuna taarifa zinasubiriwa kutoka Polisi kwa sababu kesi hiyo ina mashtaka ya kughushi. Hivyo, kutokana na hatua hiyo, Hakimu Nongwa aliahirisha kesi hiyo hadi August 30, 2017.

chanzo: millard ayo

No comments:

Post a Comment