BAADA YA MLIPUKO OFISI ZA IMMMA .POLISI YAANZA UCHUNGUZI - TANZA MEDIA ONLINE

Saturday, 26 August 2017

BAADA YA MLIPUKO OFISI ZA IMMMA .POLISI YAANZA UCHUNGUZI

Polisi Yachunguza Mlipuko Uliotokea Kwenye Ofisi za Wanasheria
 Kaimu Kamanda wa Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Lucas Mkondya amethibitisha kushambuliwa ofisi za wanasheria za IMMMA saa 8 usiku wa kuamkia leo Jumamosi, Agosti 26.

Mkondya amesema polisi wanafanya uchunguzi kujua ni nini kilihusika katika tukio hilo la mlipuko.

“Tupo hapa eneo la tukio, uchunguzi unaendelea na ukikamilika tutawapa taarifa zaidi, ila hatujajua kama bomu limehusika,” amesema Mkondya.

Ameeleza hadi sasa hakuna watu wanaoshikiliwa kuhusika na tukio hilo.

Mmoja wa viongozi wa Kampuni ya IMMMA, Sadock Magai amesema hakuna wizi ambao umefanyika katika mali zilizokuwa ndani.

“Tuwaachie Jeshi la Polisi wafanye kazi yao,” amesema Magai.

Ofisi za wanasheria wa kampuni hiyo zipo Barabara ya Umoja wa Mataifa eneo la Upanga jijini hapa.

Miongoni mwa wamiliki wa kampuni hiyo ni Fatma Karume, ambaye ni mtoto wa Rais mstaafu wa Zanzibar, Amani Abeid Karume.

No comments:

Post a Comment