KOCHA wa zamani wa Ligi Kuu ya England, Alex McLeish ameiwezesha Zamalek ya Misri kwenda hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika Jumanne.
Hiyo
inafuatia timu hiyo ya Cairo kulazimisha sare ya 1-1 na Mouloudia
Bejaia ya Algeria katuika mchezo wa marudiano hatua ya 16 Bora na
kusonga mbele kwa ushindi wa 3-1 baada ya awali kushinda 2-0 nyumbani.
Faouzi Yaya alimtungua kwa shuti la mpira adhabu kipa Mahmoud Abdel Rehim dakika ya 57 kuwaptia Bejaia bao la kuongoza.
Lakini
mfungaji wa kwenye mchezo wa kwanza, Ahmed Hamoudi akaisawazishia
Zamalek zikiwa zimebaki dakika mbili baada ya kuwatoa mabeki na
kumtungua kipa Chamseddine Rahmani.
Huo
ulikuwa ni mchezo mmoja kati ya mitatu ya marudiano iliyocheza
Jumanne-- mechi za kwanza za michuano ya Afrika kuchezwa katikati ya
wiki katika miaka 52 ya mashindano hayo ya CAF (Shirikisho la Soka
Afrika).
Maybin
Mwaba alitiokea benchi na kufunga zikiwa zimesali dakika tisa kuipa
Zesco United ya Zambia ushindi wa 2-1 dhidi ya Stade Malien ya Mali
mjini Ndola.
Wenyeji
wangeweza kupata ushindi mnono kama wa kwenye mchezo wa 3-1 mjini
Bamako wiki mbili zilizopita kama wangetumia vizuri nafasi. Mabao ya Zesco yamefungwa na Mkenya, Jesse Were ambaye angeweza kupiga hat-trick kama si kutolewa.
Washindi
wa zamani, ES Setif ya Algeria wametoa sare ya 0-0 na El Merreikh na
kusonga mbele kwa mabao ya ugenini baada ya sare ya 2-2 kwenye mchezo wa
kwanza Sudan.
Michuano hiyo itaendeela Jumatano kwa mechi kati ya;
TP Mazembe (DRC) v Wydad Athletic (Morocco), Ahly Tripoli (Libya) v
Asec Mimosas (Ivory Coast), Al Ahly (Misri) v Yanga SC (Tanzania),
Mamelodi Sundowns (Afrika Kusini) v AS Vita Club (DRC) na ES Sahel
(Tunisia) v Enyimba (Nigeria)
Zamalek imefuzu hatua ya makundi Ligi ya Mabingwa Afrika |
No comments:
Post a Comment