Tuddy Thomas alia majambazi waliofanya sasa ashindwe kupiga kinanda vizuri - TANZA MEDIA ONLINE

Saturday 20 February 2016

Tuddy Thomas alia majambazi waliofanya sasa ashindwe kupiga kinanda vizuri

tuddy

Prodyuza Tuddy Thomas toka studio za Epic rekodi amefunguka na kusema kwa sasa anapata wakati mgumu sana kupiga kinanda,hiyo inatoka na maumivu aliyo nayo baada ya kuvamiwa na majambazi katikati ya mwaka jana na kupata majeraha kadhaa.
Hakuna kitu kinaniuma kama upigaji wa kinanda vizuri,nimekuwa sina uwezo wa kupiga kinanda vizuri nakuwa nadokoa sana,kama nyimbo nilikuwa napiga kwa dakika tano sasa hivi nafanya kwa lisaa na nusu…Sometime huwa nikikaa kufikiria nalia sana” amefunguka Tuddy.a
Hata hivyo Tuddy amemshukuru msanii Diamond kwa kumtia moyo na kumwamini na kumfanya aweza kupiga kinanda vizuri kwenye wimbo wa Je Utanipenda.”Wakati nafanya kazi na Diamond,Je Utanipenda nilimwita Emma aje apige kinanda ila Diamond akanambia,unajua Tuddy unatachi za peke yako,akataka nipige vile vile japo ilikuwa kidogo na kwa ugumu“aliongeza Prodyuza huyo na kuwashukuru wasanii wanaoendelea kumwamini.
Source: Clouds

No comments:

Post a Comment