The Game na Lloyd Banks wamaliza beef yao,50 Cent hajafurahishwa na hili. - TANZA MEDIA ONLINE

Saturday 20 February 2016

The Game na Lloyd Banks wamaliza beef yao,50 Cent hajafurahishwa na hili.

50Cent
50 Cent hajafurahishwa na kupatana kwa The Game na Lloyd Banks. Rapa Kutoka Compton The Game ameweka picha ya kuonyesha kuwa yeye na rapa wa G Unit ‘ Lloyd Banks’ wamepatana na mambo yako shwari.
Wasanii hawa walikutana Dubai na picha yao pamoja iliambatana na ujumbe wa “Still.” Rapa 50 Cent ambaye hana maelewano mazuri na The Game hajafurahishwa kabisa na issue hii.
banks
“Nikiona hii picha naona CONFUSION TU, nadhani sio mimi tu, sitaki matatizo na sina tatizo na hawa wawili kufanya hivi, ila kuna washkaji ambao hawata penda hii” 50 Cent hapa anamaanisha beef kubwa kati yake Game si muziki tu ila ni mauwaji ya msanii wa G Unit wa zamani aliyeuwawa na watu wa karibu wa The Game na meneja wake, 50 Cent anamuongelea hapa Lodi Mack member wa G-Unit ambaye jina lake ni Lowell Fletcher aliuwawa mwaka 2009 na mwaka 2014, aliyekuwa meneja wa Jimmy “Henchman” Rosemond alikutwa na hatia na kufungwa kifungo cha maisha”

No comments:

Post a Comment