MNYAMA ACHINJWA MARA MBILI NA WANA WA JANGWANI - TANZA MEDIA ONLINE

Saturday 20 February 2016

MNYAMA ACHINJWA MARA MBILI NA WANA WA JANGWANI

Wachezaji wa Yanga wakiongozwa na Simon Msuva (katikati) wakishangilia ushindi wao wa bao 2-0 dhidi ya Simba kwenye mchezo wa Dar Derby uliopigwa kwenye uwanja wa taifa February 20, 2016
Wachezaji wa Yanga wakiongozwa na Simon Msuva (katikati) wakishangilia ushindi wao wa bao 2-0 dhidi ya Simba kwenye mchezo wa Dar Derby uliopigwa kwenye uwanja wa taifa February 20, 2016
Yanga imefuta rekodi ya kocha Jackson Mayanja ya ushindi mfululizo baada ya kupata ushindi wa bao 2-0 dhidi ya Simba mchezo wa ligi kuu ya Vodacom uliozikutanisha timu hizo kwenye mchezo wa marudiano.
Ushindi huo ni wa pili kwa Yanga dhidi ya Simba ndani ya msimu huu wa 2025-16 baada ya awali kupata ushindi kama huo kwenye mchezo wa raundi ya kwanza.
Beki wa kushoto wa Simba SC Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ akimtoka beki wa kulia wa Yanga Juma Abdul
Beki wa kushoto wa Simba SC Mohamed Hussein ‘Tshabalala’ akimtoka beki wa kulia wa Yanga Juma Abdul
Bao la kwanza la Yanga limefungwa na Donald Ngoma dakika ya 39 baada ya Hassan Kessy kutoa pasi fupi kwa golikipa wake Vicent Agban ambayo ilinaswa na mzimbabwe huyo na kuwekwa kambani mapema kipindi cha kwanza.
Yanga walipata bao la pili kutoka kwa nyota wa mchezaji wa zamani wa Simba Amis Tambwe dakika ya 72 kipindi cha pili.
Adbi Banda akiwaungia mkono mashabiki wa Simba mara bada ya kutolewa nje ya mchezo kwa kadi nyekundu na mwamuzi Jonesi Rukyaa kufuatia kuoneshwa kadi mbili za njano
Adbi Banda akiwaungia mkono mashabiki wa Simba mara bada ya kutolewa nje ya mchezo kwa kadi nyekundu na mwamuzi Jonesi Rukyaa kufuatia kuoneshwa kadi mbili za njano
Rekodi unazotakiwa kujua
  • Yanga ndiyo timu ya kwanza kuifunga Simba tangu iwe chini ya kocha Jackson Mayanja tangu kocha huyo atangazwe kuchukua mikoba ya Dylan Kerr.
  • Simba ilikuwa haijafungwa zaidi ya goli moja tangu iwe chini ya Mayanja, Yanga wamekuwa timu ya kwanza kuifunga Simba zaidi ya goli moja baada ya kuifunga bao 2-0.
Raha ya ushindi, mashabiki wa Yanga wakishangilia ushindi wao wa bao 2-0 dhisi ya Simba
Raha ya ushindi, mashabiki wa Yanga wakishangilia ushindi wao wa bao 2-0 dhisi ya Simba
  • Amis Tambwe ni mchezaji pekee katika msimu huu kuifunga timu yake ya zamani katika mechi mbili ndani ya msimu mmoja.
  • Amis Tambwe, Hamisi Kiiza na Ally Mustafa ni wachezaji ambao leo walikuwa wanacheza dhidi ya timu zao za zamani. Wachezaji hao wamewahi kucheza kwenye vilabu hivyo kwa nyakati tofauti kisha kuhamia kwenye upande pinzani.
  • Yanga inapanda kileleni mwa ligi kwa mara nyingine baada ya kufikisha pointi 46 ikiwa imecheza michezo 19 ikifuatiwa na Simba yenye pointi 45 baada ya michezo 20.
Mashabiki wa Yanga waksaidia kumshusha shabiki mwenzao aliyepoteza fahamu ili apatiwe huduma ya kwanza
Mashabiki wa Yanga waksaidia kumshusha shabiki mwenzao aliyepoteza fahamu ili apatiwe huduma ya kwanza
  • Yanga imeshinda kwa mara ya kwanza kwenye uwanja wa taifa baada ya mechi mbili za ugenini. Ilifungwa 2-0 na Coastal Union kwenye uwanja wa Mkwakwani-Tanga kabla ya kutoka sare ya bao 2-2 kwenye uwanja wa Sokoine Mbeya dhidi ya Tanzania Prisons.
Mashabiki wa Simba wakiwa wametulia jukwaani baada ya kupigwa bao mbili na watani zao wa jadi YangaMashabiki wa Simba wakiwa wametulia jukwaani baada ya kupigwa bao mbili na watani zao wa jadi Yanga
  • Magoli ya mechi ya leo yamefungwa na wachezaji wa kigeni Donald Ngoma (Zimbabwe) na Amis Tambwe (Burundi).
  • Simba imefungwa na Yanga kwenye mechi zote (mbili) za msimu huu (2-0) 26 September, 2015, (2-0) 20 February, 2016.
Nini Kinafuata kwa timu hizo baada ya mchezo wa leo?
Simba itakuwa mwenyeji wa Mbeya City March 6, 2016 kwenye mchezo wao ujao wa VPL kwenye uwanja wa taifa.
Yanga wataialika Mtibwa Sugar kwenye mchezo unaofuata katika liga, mchezo huo utapigwa kwenye uwanja wa taifa February 24, 2016.
source : http://shaffihdauda.co.tz

No comments:

Post a Comment