Dakika
90 za Mtanange wa Watani wa Jadi, Simba na Yanga zimemalijika jioni hii
hapa uwanja wa Taifa, Jijini Dar es Salaam kwa kutoka kifua mbele kwa
timu ya Yanga baada ya kuchapa Simba bao 2-0. Magoli ya mchezo huo
yametiwa kimiani na washambuliaji Donald Ngoma (Dakika ya 38 kipindi cha
kwanza) na goli la pili limefungwa na Amissi Tambwe (Dakika ya 34
kipindi cha pili) na kufanya matokeo kubaki hivyo hadi mwisho wa
mchezo.PICHA NA OTHMAN MICHUZI - MMG.
Mshambuliaji
wa Timu ya Yanga, Donald Ngoma (11) akimpiga chenga Golikipa wa Timu ya
Simba, Vicent Angban na kupachika bao la kwanza kwa timu yake wakati wa
Mtanange wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kati ya Yanga na Simba,
uliomalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es salaam.Yanga
imeshinda Bao 2-0.
Mshambuliaji
wa Timu ya Yanga, Donald Ngoma akishangilia Goli aliloipatia timu yake,
wakati wa Mtanange wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kati ya Yanga
na Simba, uliomalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es
salaam.Yanga imeshinda Bao 2-0.
Mashabiki wa timu zote mbili waliwa wamefurika kwa wingi ndani ya uwanja wa Taifa.
Golikipa wa Timu ya Simba, Vicent Angban akiwa amejiweka tayari kuokoa mpira uliokuwa ukielekezwa langoni kwake.
Mshambuliaji wa Timu ya Yanga, Haruna Niyonzima akijaribu kumtoka Beki wa Timu ya Simba, Kessy Ramadhan, wakati
wa Mtanange wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, kati ya Yanga na
Simba, uliomalizika jioni hii kwenye Uwanja wa Taifa Jijini Dar es
salaam.Yanga imeshinda Bao 2-0.
Mashabiki wa Yanga baada ya Ushindi.
Mashabiki wa Simba baada ya kuchapwa.
No comments:
Post a Comment