Njia Sita Za Kushinda na Kufaidika na Beef La Muziki. - TANZA MEDIA ONLINE

Saturday 30 January 2016

Njia Sita Za Kushinda na Kufaidika na Beef La Muziki.


beef

Rap ndio muziki unaochukua namba moja kwenye orodha ya aina ya miziki yenye mikwaruzano ya wasanii [Beef]. Mifano hai ni kama East Coast vs West Coast, Jay-Z vs Nas, Ja Rule vs 50 Cent,hapa Tanzania East Coast vs TMK , Wanaume halisi vs Wanaume family , Madee vs Ney wa mitego , Madee vs Afande sele, Diamond vs Ali Kiba.
Hizi ndio njia sita za kushinda beef la muziki
1. Kuwa na beef na msanii mkubwa zaidi yako, mwenye mashabiki wengi zaidi ila sio mkali sana.
50 Cent alivyoanzisha beef na Ja Rule alijuwa kuwa Ja ni mkubwa New York, yeye ataonekana rapa anayejiamini kwenda dhidi yake na kushinda. Pia Ja Rule na lebel ya Murder Inc ilikuwa inaelekea pabaya na ndicho kilichompa 50 Cent advantage.
2. Tumia point zisizojulikana kuhusu yeye kumchafua.
2 Pac alivyo rap kuhusu kuwa na mahusiano na mke wa B I G, kitendo kilimgusa sana BIG na watu wake. Filamu ya maisha ya BIG Ilionyesha kuwa alimpiga Faith Evans baada ya kusikia aliwahi kuwa na mahusiano na 2 Pac. Watu hawakujua kuwa kitu kama hicho kiliwahi kutokea, ikawa aibu kwa BIG. ilikuwa kwenye wimbo wa Hit Em Up.
3. Wimbo wako wa beef uwe kwenye mixtape na utambulishe kwenye radio kubwa mjini.
Kutambulisha wimbo wa beef na kumchana msanii mwenzako ni kuthubutu kuwa juu yake kama hatajibu, na mara nyingi kwenye hiphop na rap lazima jibu litatoka ata kama wasanii watakana kuwa sio jibu na halimlengi hasimu wake.
4. Usikutane na hasimu wako uso kwa uso/ msipigane
Miaka ya kupigana na kuumizana imepitwa na wakati, sasa ni mashairi na uwezo wa kufanya kazi, kubali kufanya nae tamasha au freestyle battle kwenye radio au tv. Usimtafute mtaani au kwenye sehemu za starehe.
5. Hakikisha una wimbo mkali unaotoka baada ya wimbo wa beef kutoka.
Kama huna wimbo mkali studio tayari kutoka baada ya beef yako, hata usijisumbue kuwa na beef sababu baada ya beef utabaki kimya na mpinzani wako atakufunika. mpango mzima ni wewe umtumie kuwa maarufu na kushika mashabiki wake so be ready.
6. Beef itakuongezea wafuasi kwenye mitandao yako ya kijamii,
Kuwa tayari kuona mafanikio ya beef, watu watataka kujua kazi zako, kuwa na video bora, muonekano wako uwe bora, jiweke karibu na vyombo vya habari, kuwa huru kufanya mahojiano.

No comments:

Post a Comment