“
Siku ya January 7, 2015 itabaki kuwa siku ya kukumbukwa na Mbwana Ally Samatta kwenye maisha yake yote kufuatia kuandika rekodi mpya barani Afrika na Tanzania baada ya kutangazwa mshindi wa tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani kwenye sherehe za ugawaji tuzo za Glo-Caf Awards zilizofanyika Abuja, Nigeria.
Shaffihdauda.co.tz imepiga story na Mbwana Samatta muda mfupi baada ya kutangazwa mshindi wa tuzo hiyo, Samatta amei-dedicate tuzo hiyo kwa babayake mzazi pamoja na familia kwa ujumla lakini hakuwasahau watanzania waliokuwa nyuma yake kumwombea na kumtakia kila la kheri ili atwae tuzo hiyo.
Shaffihdauda.co.tz: Hongera sana Samatta kwa kufanikiwa kutwaa tuzo hii na kuipeperusha bendera ya Tanzania, unajisikiaje kuwa mshindi wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika based on Africa?
Shaffihdauda.co.tz: Nakosa la kusema kwakweli, kwa jinsi watanzania walivyokuwa wameniombea na kwa tuzo hii sijui hata nisemaje ili kuwashukuru au sijui nifanyaje kuwashukuru ili wajue kweli nawapenda na niko nao pamoja kwasababu ya maombi na jinsi walivyokuwa wanaonesha imani hata ambayo mimi mwenyewe sikuwanayo kwenye hii tuzo.
Lakini pia sidhani kama naweza kumsahau Rais mstaafu aliyepita Mh. Jakaya Mrisho Kikwete kwa inspiration ambayo alinipa siku moja ambayo tulikutana nchini Congo DR aliniambia mambo mengi sana ambayo kwa kiasi kikubwa yalini-motivate. Unajua mtu kama Rais anakuja anakwambia mambo ambayo yanakuhusu moja kwa moja na taifa ni jambo kubwa.
Shaffihdauda.co.tz: Alikwambia maneno gani?
Mbwana Samatta: Ni mengi tulizungumza lakini moja alituambia mimi na Thomas kwamba, tumeonesha njia tusikubali kubakia Afrika tujitahidi kwenda kucheza Ulaya ili kuonesha njia kwa vipaji vingine ambavyo viko nyumbani. Alisema nyinyi ndio icons wetu, watanzania karibu wote tunawategemea nyinyi kwenye medani ya soka, mjitahidi msituangushe.
Sidhani kama hata wewe mwenyewe nikikwambia unachukuliaje lakini ni maneno ambayo kwa kiasi kikubwa yalini-push kwa kuona ikiwa Rais anasema hivi, je familia yangu au watu wa karibu pamoja na sehemu niliyotokea wanachukuliaje hili suala lakini ilinipa morali na kusema kweli inabidi nifanye vizuri. Kweli nashukuru Mungu amenisaidia.
Shaffihdauda.co.tz: Tuzo hii inamaana gani kwenye career yako ya mchezo wa soka?
Mbwana Samatta: Tuzo hii inamaana sana sana, kiasi cha kwamba ni vigumu kuielezea kwasababu tumeona wachezaji wengi wa kiafrika ambao wako Ulaya wanapata mafanikio mengi Ulaya lakini hawana tuzo kama hii lakini hiki ni kitu ambacho sitakuja kukisahau kwenye maisha yangu. Sijui nikuelezeaje ili uweze kunielewa au watanzania waweze kunielewa lakini kwangu mimi inamaana kubwa sana. Sijawahi yani kujihisi hivi kwenye maisha yangu, sijawahi kuwa katika hali hii.
Shaffihdauda.co.tz: Wakati unakua unaanza kucheza mpira, uliwahi kuwaza siku moja katika maisha yako ingeweza kutokea siku kama ya leo?
Mbwana Samatta: Kwakweli sikuwahi kufikiria yani kama ipo siku nitashinda tuzo yenye heshima kama hii,yani kwakweli sijui.
Shaffihdauda.co.tz: Unahisi nini kimesababisha kitu kama hiki leo kuweza kutokea?
Mbwana Samatta: Mimi nafikiri ni kujituma kwasababu wakati mwaka unaanza kuna baadhi ya rafiki zangu nilikuwa nawaambia nataka mwaka 2015 uwe mwaka ambao sitoweza kuja kuusahau kwenye maisha yangu. Mungu mkubwa wakati mwaka unaanza ari yangu ya kiufungaji na kiuchezaji ilikuwa chilni lakini kitu ambacho kiliweza kunifanya nirudi kwenye ari ni jitihada. Baada ya kuona kwamba hali si nzuri niliongeza sana jitihada katika mazoezi pamoja na kupangilia muda wangu wa kupumzika.
Shaffihdauda.co.tz: Mbwana wewe ni mshindi umekaa sehemu moja na wachezaji waliofanikiwa sana katika level ya juu. Umekaa na Yaya Toure, Andre Ayew na Pierre-Emerick Aubameyang ambaye ametwaa tuzo ya Mwanasoka bora wa Afrika. Unadhani katika siku zijazo unaweza ukachukua tuzo kama aliyochukua Aubameyang?
Mbwana Samatta: Baada ya kupata tuzo hii naweza nikasema naweza kuchukua hiyo tuzo na ni kitu ambacho kitaleta historia kuchukua mchezaji bora wa Afriaca based in Africa halafu ukachukua tena mchezaji bora wa Afrika ni kitu ambacho ni vigumu kutokea lakini nafikiri naweza ni jitihada, kuomba Mungu na kuheshimu kazi.
Shaffihdauda.co.tz: Nakumbuka ile medal yako ya ubingwa wa Afrika ulii-dedicate kwa mamayako mzazi ambaye kwa bahati mbaya hatunaye duniani. Tuzo hii ya mchezaji bora Afrika kwa wachezaji wa ndani unai-dedicate kwa nani?
Mbwana Samatta: Nina ma-group mawili au matatu ya ku-dedicate hii tuzo, kwanza tuzo hii nai-dedicate moja kwa moja kwa babayangu mzee Aly Samatta kwasababu kila siku amekuwa ananiunga mkono katika career yangu na maisha yangu ya soka pamoja na familia kiujumla pili nai-dedicate tuzo hii kwa Mh. Rais mstaafu Jakaya Mrisho Kikwete kwa maneno yake aliyoniambia na kwa jinsi ambavyo alinipa hamasa.
Lakini tatu ni ya watanzania wote kwa jinsi walivyoniombea na jinsi ambavyo walikuwa wakipenda na kuhitaji mimi nichukue tuzo hii, kwahiyo nadhani tuzo ni yao.
Shaffihdauda.co.tz: Mwambie maneno matatu kijana wa kitanzania ambaye ana-ndoto za kufikia mafanikio uliyonayo hadi sasa.
Mbwana Samatta: Maneno yangu matatu nayoweza kumwambia kijana wa kitanzania ni haya; Jitume, Heshimu, Utapata.
tangazaji namba moja wa michezo Tanzania.
chanzo : shafih dauda
No comments:
Post a Comment