KULIKONI TWIGA STARS, HADI KAIJAGE AJIUZULU !!?? - TANZA MEDIA ONLINE

Friday 8 January 2016

KULIKONI TWIGA STARS, HADI KAIJAGE AJIUZULU !!??


Aliyekuwa kocha mkuu wa Twiga Stars na Tanzanite Rogasian Kaijage akiwa na wachezaji wake wakati akiwa kocha wa timu hiyo
Aliyekuwa kocha mkuu wa Twiga Stars na Tanzanite Rogasian Kaijage akiwa na wachezaji wake wakati kabla ya kujiuzulu
Kocha mkuu wa timu za taifa za mpira wa miguu za wanawake ‘Twiga Stars’ na ile ya ‘Tanzanite’ Rogasian Kaijage amejiuzulu kuzifundisha timu hizo kwa madai kwamba mazingira hayampi mwanya wa kuzisaidia timu hizo hivyo ameamua kukaa pembeni.
Kocha huyo kajiuzulu kwa kuandika ujumbe mzito kwenye moja ya mitandao ya kijamii akiwaasa wachezaji wake kupambana na kutokata tamaa kutokana na kujiuzulu kwake.
“Wanangu na wajukuu zangu wa Twiga na Tanzanite, nasikitika sana kwaacha njiani. Lakini imebidi iwe hivyo kwasababu mazingira hayanipi mwanya wa kuwasaidia kupata maendeleo niliyokusudia”, ujumbe huo unasomeka hivyo.
“Nawaomba msikate tamaa muongeze bidii Mungu atawasaidia, nami bado nitakuwa nanyi muda wote”. 
“Bora nitafute njia za kuweza kuwasaidia nikiwa nje ya timu. Kumbuka ilimbidi Yesu afe ili watu wakombolewe, hivyo na mimi inanibidi nitoke ili kuamsha ukombozi wenu. Bado niko nanyi. Nawapenda sana”.
Haya hapa maneno ya aliyekuwa kocha wa Twiga Stars na Tanzanite
Kaijage 11
Hayo ni maneno mazito kutoka kwa Kaijage kwenda kwa wachezaji wake wa timu ya Twiga Stars na Tanzanite.

No comments:

Post a Comment