
Rais wa Tanzania Dkt John Magufuli amewataka raia nchini humo kuwapuuza wanaodai Serikali inakopa sana. Kiongozi huyo alisema mikopo inayochukuliwa na taifa hilo ina manufaa na itachochea ukuaji wa uchumi.
Dkt
Magufuli alikuwa akihutubu alipokuwa anaifungua rasmi barabara ya lami
ya Iringa - Migoli - Fufu yenye urefu wa kilometa 189.Barabara
hiyo inaunganisha Mkoa wa Iringa na Mkoa wa Dodoma na Barabara hiyo
ambayo ni sehemu ya barabara kuu ya kuanzia Cape Town nchini Afrika
Kusini hadi Cairo nchini Misri (The Great North Road).
Ujenzi
wa barabara hiyo uligharimu Shilingi Bilioni 207.457 ikiwa ni ufadhili
wa benki ya maendeleo ya Afrika (AfDB) kwa asilimia 65.9, Shirika la
Maendeleo la Kimataifa la Japan (JICA) kwa asilimia 21.3.
Serikali ya Tanzania ilitoa asilimia 12.8.Tanzania
imekuwa ikikopa kutoka kwa mashirika ya kimataifa kufadhili miradi
mingi ya miundo mbinu ikiwemo miradi ya barabara na reli.
Ripoti
ya mwaka wa kifedha wa 2016/2017 ripoti ya Bank Kuu ya Tanzania
inaonesha deni la taifa hilo limefikia Dola 23.78 bilioni (zaidi ya
Sh52.29 trilioni).
Deni hilo liliongezeka kwa asilimia 9.1 katika mwaka huo ulianza Juni 2016. Hata hivyo, serikali imesisitiza kwamba kiwango hicho cha deni badi hakijapita kiwango kinachokubalika kimataifa. Deni hilo ni sawa na asilimia 48.9 ya pato la Taifa, kwa mujibu wa ripoti hiyo ya BOT.
Sehemu kubwa ya deni hilo ni kutoka kwa wakopeshaji wa nje ambao wameikopesha Tanzania dola za Marekani bilioni 18.5.
Kiasi
hicho kiliongezeka kwa asilimia 8.9 ukilinganisha na kiwango cha deni
mwaka uliodangulia ambapo deni lilikuwa dola za Marekani bilioni 16.4.
Baadhi ya wachanganuzi wameikosoa hatua ya serikali kukopa kiasi
kikubwa cha fedha lakini Dkt Magufuli amesema hakufai kuwa na wasiwasi
wowote.
Akihutubu Iringa, Rais huyo alisema na fedha hizo hukopwa
kwa masharti nafuu, riba ndogo na hulipwa kwa muda mrefu, na kwamba
ndizo zinatumika kujenga miundombinu ya kuchochea uchumi.
Wakati
wa kuadhimisha miaka 54 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar katika
sherehe zilizofanyika uwanja wa Jamhuri jijini Dodoma, kiongozi huyo
alieleza matumaini kwamba uchumi wa Tanzania utatengemaa.
"Taifa
letu linakwenda vizuri, uchumi wetu unakua vizuri, mwaka jana umekuwa
kwa wastani wa asilimia 7 na mwaka huu tunatarajia utakua kwa wastani wa
asilimia 7.1, mfumuko wa bei umeendelea kuwa chini kwa wastani wa
asilimia 4," alisema.
Baadaye alikutana na kufanya mazungumzo na Rais wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (AfDB) Dkt Akinumwi Adesina.
Taarifa
iliyotolewa na ikulu ilisema Dkt Adesina alimpongeza Mhe. Rais Magufuli
kwa kazi kubwa anayoifanya kuimarisha uchumi wa Tanzania na kusema
wamejadiliana mambo kadhaa yakiwemo namna benki hiyo ilivyosaidia juhudi
za maendeleo za Tanzania tangu mwaka 1971 na inavyoendelea kusaidia
katika ufadhili wa miradi mbalimbali ya maendeleo.
Alitaja baadhi
ya maeneo ambayo AfDB itatoa ufadhili kuwa ni uzalishaji na usambazaji
wa nishati, uboreshaji wa miundombinu ikiwemo ujenzi wa miundombinu ya
Jiji la Dodoma hasa barabara.
"Yote kwa yote nimemhakikishia Rais
Magufuli kuwa AfDB itamuunga mkono katika mipango yake na maono yake ili
tuweze kuisaidia Tanzania kukua zaidi, nimefurahi kuzungumza na Mhe.
Rais na naona Tanzania ipo katika njia sahihi," alisema Dkt Adesina kwa
mujibu wa taarifa hiyo ya ikulu.
Kwa mujibu wa Dkt Magufuli, AfDB
imefadhili miradi ya maendeleo yenye thamani ya Dola za Marekani Bilioni
3.457 (sawa na Shilingi Trilioni 7.78 Tanzania) zikiwemo fedha za
miradi 25 zilizotolewa kuanzia mwezi Novemba, 2017 yenye thamani ya Dola
za Marekani Bilioni 1.986 (Shilingi Trilioni 4.47 Kitanzania).
Chanzo:bbcswahili
No comments:
Post a Comment