Leo Tarehe 18 April 2018,Halmashauri Ya Manispaa ya
Ubungo,Imeingia Mkataba wa Makabidhiano na Kutoa Huduma ya Mikopo ya
Wanawake,Vijana na walemavu na Benki ya CRDB,Kwa Niaba ya Halamshauri.
Mstahiki meya,Boniface Jacob ametiliana Saini ya Mkataba na Benki ya CRDB ambapo wametiliana saini Ya utoaji wa Huduma hiyo.Fedha za Kuanzia Shughuli hiyo Kiasi cha Shillingi
Billioni 1.947 Zitapelekwa Benki ya CRDB kwa ajili ya Ugawaji wa Fedha
hizo kwenye Vikundi Mbalimbali vya wanawake(40%) Vijana(40) na
walemavu(20)
Ambapo kiasi kikubwa Billioni 1.947 kitaifanya Halamshauri
Kuvunja Rekodi kwa Kuwa Halmashauri Ya kwanza DSM na Tanzania kuwahi
kutoa kiasi kingi cha fedha kwa ajili ya Mikopo ya Vijana,wanawake na
kundi Maalum la walemavu
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo,Bw.John
Kayombo,ameeeleza kuwa fedha hizo ni sehemu ya asilimia 10,za Mapato ya
ndani yaliyokuwa yakitengwa na Halmashauri,Kwa Muda wa Mwaka
Mmoja,Pamoja na fedha za Mgawanyo wa Halamshauri kutoka Manispaa ya
Kinondoni.
Aidha Mstahiki Meya,Boniface Jacob Ameeleza kuwa;
Halamashauri Ya Manispaa ya Ubungo imefikia hatua ya kutiliana Saini na
Benki ya CRDB baada ya Kushindanisha Mabenki yote ya Tanzania,na
Kuangalia Benki yenye Huduma Nzuri kwa wajasiriamali wake,itakayo
kubali kutoa Riba ndogo kwa Wajasiriamali,Na kukubali kuchangia shughuli
za Utoaji Huduma hiyo ya kukagua na kuvisaidia Vikundi vya wakopaji.
Mpaka Leo wakina mama 11,312 na Vijana 1,224 wameshajaza
fomu za Maombi ya Mikopo kutoka Halmashauri,kwa kata zote 14 na Mitaa
91 ,Huku wito ukitolewa kwa vijana baada ya Idadi Ndogo ya Vijana
kujotokea kulinganisha na akina Mama.
MWISHO.
Mstahiki meya Amewashukuru Wataalamu wakiongozwa na Mkurugenzi,wabunge na Madiwani wote,kwa Ushirikiano na Jitihada za Kuibadilisha Manispaa ya Ubungo
Mstahiki meya Amewashukuru Wataalamu wakiongozwa na Mkurugenzi,wabunge na Madiwani wote,kwa Ushirikiano na Jitihada za Kuibadilisha Manispaa ya Ubungo
IMETOLEWA Na
OFISI YA MSTAHIKI MEYA
MANISPAA YA UBUNGO - 18-04-2018
OFISI YA MSTAHIKI MEYA
MANISPAA YA UBUNGO - 18-04-2018
No comments:
Post a Comment