Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Prof. Makame Mbarawa amezindua ujenzi wa reli ya juu yenye urefu wa kilometa 300 itakayojengwa kuanzia Shaurimoyo jijini Dar es salaam.
Amesema kuwa reli hiyo ya juu inalenga kuondoa msongamano wa magari ambapo yatapita chini huku treni ikipita juu.
Aidha, Mbarawa amewataka wananchi wenye majengo yaliyopo pembezoni mwa reli kuyabomoa wenyewe huku akiwasisitiza kutovamia hifadhi ya reli.
“Tumeanzisha ujenzi huu wa reli ya kisasa kwa kipande hiki cha Dar es salaam ambacho tunategemea hadi julai 2019 kitakuwa kimekamilika, kwani kuna changamoto nyingi,” amesema Prof. Mbarawa
Hata hivyo, katika mradi wa awamu ya kwanza, makandarasi wapo Msoga, Ngerengere na Dar es salaam, huku awamu ya pili ikitarajiwa kuanzia Morogoro hadi Makutupora.
Miradi hiyo itagharimu shil. Trilioni 7.6 hivyo Prof. Mbarawa amewataka makandarasi na mshauri wa mradi kuhakikisha wanasimamia ipasavyo ujenzi huo ili ukamilike kwa muda uliopangwa.
No comments:
Post a Comment