Viongozi wa Korea Kaskazini na Korea Kusini wanatarajiwa kufanya mkutano mwezi ujao, kwa mujibu wa Korea Kusini.Utakuwa
mkutano wa kwanza wa aina hiyo kwa zaidi ya miaka 10 na wa kwanza
tangu Kim Jong-un aingie madarakani nchini Korea Kaskazini.Ujumbe
huo pia ulisema Bw Kim alisema kjwa angependa kuzungumza kuhusu
kuachana na silaha za nyuklia ikiwa tu atahakikishiwa usalama wa nchi
yake.
Bw Kim na rais wa Korea Kusini Moon Jae-in, watakutana kwennye
mpaka wenye ulinzia mkali mwezi ujao katika kijiji cha mapatano cha
Panmunjom. Nchi hizo pia zilikubaliana kufungua mawasiliano ya simu kati
ya viongozi hao.
Baada ya kurejea kutoka ziara hiyo isiyo ya
kawaida, maafisa wa Korea Kusini walisema Bw Kim aliwaaambia kuwa
hakutakuwa na majaribio ya makombora wakati mazungumzo yakiendelea.Haya ni mabadiliko makubwa kwa kiongozi wa Korea Kaskazini kulingana na mwandishi wa BBC Laura Bicker kutoka Seoul.
Marekani inasema kuwa mazungumzo na Korea Kaskazini
yataendelea tu ikiwa tu itakuwa tayari kuzungumzia suala la kuondoa
silaha za nyuklia.Wakati wa mashindano ya Olimpiki Korea
Kaskazini na Kusini walionyesha urafiki kwa kutuma wanariadha kushindana
kama kikosi kimoja na kufanya mazungumzo.
Lakini Marekani
inashikilia msimamo wake kuwa mbinu za Korea Kaskazini zitakuwa na uzito
mdogo bila ya kujitolea kwenye suala la silaha za nyuklia hasa
kutokana na majaribio ya mwaka uliopita ya nyuklia na makombora
yaliyofanywa na Korea Kaskazini.
Maafisa wa Korea Kusini walishiriki chakula cha jioni na Kim
Jong-un siku ya Jumatatu. Kati ya ujumbe huo alikuwa mkuu wa ujasusi
Hoon na mshauri wa masuala ya usalama wa taifa Chun Eui-yong.
Wao
ni maafisa wa kwanza wa Korea Kusini kukutana naBw Kim tangu aingie
madarakani. Walerejea mjini Seoul siku ya Jumanne asubuhi.Ujumbe
wa Korea Kusini unatarajiwa kuzuru Marekani baadaye wiki hii
kuwajulisha maafisa wa Marekani kuhusu mazungumzo kati yao na Korea
Kaskazini.
No comments:
Post a Comment