Jeshi la Polisi Zanzibar limesema kuwa halina taarifa za
kuonekana kwa mashekhe watatu wa Jumuiya ya Maimamu Zanzibar, ambao
waliripotiwa kutoonekana tangu Januari 9, mwaka huu.
Hayo yamesemwa na Kamanda wa Polisi, Mkoa wa Mjini Magharibi, Hassan
Nassir Ali, alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari, ambapo amesema
kuwa jeshi hilo lilifanya kazi ya kuwatafuta mashekhe hao, lakini
halikufanikiwa kuwaona.
“Zipo taarifa mitaani kuwa mashekhe hao wameonekana sasa nashangaa
kwanini waliokuja kuripoti kuwa hawaonekani wameshindwa kuja kutoa
taarifa kuwa wameonekana,” amesema Kamanda Ali.
Aidha, Kamanda huyo ameiasa jamii kuacha kuchanganya mambo ya
kihalifu na kisiasa kwa kuwa halileti taswira nzuri kwa jamii na taifa
kwa ujumla.
Hata hivyo, Kamanda Ali ameongeza kuwa awali jeshi hilo lilipokea
taarifa rasmi kutoka kwa familia na ndugu wa mashekhe hao, kuwa
hawaonekani na wamepotea katika mazingira ya kutatanisha huku
likihusishwa jeshi hilo kuwa ndio lililo wachukua.
No comments:
Post a Comment