Wafuasi Chadema Waliokamatwa kwa Maandamano wafikishwa Mahakamani - TANZA MEDIA ONLINE

Thursday, 22 February 2018

Wafuasi Chadema Waliokamatwa kwa Maandamano wafikishwa Mahakamani


Watu 28 wanaodaiwa kuwa wafuasi wa Chadema wamefikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu wakituhumiwa kufanya mkusanyiko usio halali na kinyume na sheria.

Washtakiwa hao wamefikishwa mahakamani hapo mbele ya hakimu mkazi, Godfrey Mwambapa na kusomewa shtaka la kufanya mkusanyiko usiyo halali.

Washtakiwa kwa pamoja wanadaiwa walitenda kosa hilo Februari 16, 2018  katika barabara ya Kawawa eneo la Mkwajuni wilayani Kinondoni.


Washtakiwa hao wote kwa pamoja Wamekana shtaka hilo na kurudishwa rumande baada ya kushindwa kutimiza masharti ya dhamana ya kuwa na mdhamini mmoja atakayesaini hati ya Sh1.5milioni kwa kila mmoja.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Machi 3, 2018 itakapotajwa tena. 

No comments:

Post a Comment