Matangazo ya vituo viwili vya televisheni Kenya yarejea hewani - TANZA MEDIA ONLINE

Tuesday, 6 February 2018

Matangazo ya vituo viwili vya televisheni Kenya yarejea hewani


Studio ya TV haina watuHaki miliki ya pichaREUTERS
Image caption

Lakini bado haviwezi kutazamwa na Wakenya wengi ambao hawana king'amuzi.
Kupitia mtandao wao wa Twitter, NTV wamesema wamerudi hewani kwenye ving'amuzi vya "Dstv, GoTV and Zuku baada ya kufungiwa na serikali."
Stesheni ya iliyokuwa mmojawapo zilizoathirika na hatua ya serikali ,Citizen TV bado haijafunguliwa.
Serikali ilizifunga stesheni tatu za televisheni NTV, Citizen na KTN kwa madai kuwa vilipanga kupeperusha moja kwa moja matangazo sherehe ya kumuapisha kiongozi wa upinzani Raila Odinga kama rais licha ya onyo kutofanya hivyo.
KTN news presenter on airHaki miliki ya pichaKTN
Image caption
Awali, wanaharakati waliokuwa wakiandamana kuishinikiza serikali kuvifungua vituo hivyo, walitawanywa na polisi kwa kutumia gesi ya kutoa machozi
"Hii si mara ya kwanza tumiona serikali ya Jubilee ikiangamiza haki za waandishi wa wahabari. Tumeona ikifanyika kwa muda mrefu"
Tom Oketch mmojawapo wa waandalizi wa maaandamano hayo ameiambia BBC .
"Hawa heshimu sheria, hawa heshimu katiba, wananchi wa Kenya hawatawaruhusu kuturidisha katika enzi za Jomo Kenyatta, enzi za Moi, tutapigana nao mpaka mwisho" ameelezea Tom.
Wiki iliyopita,Mahakama Kuu nchini humo iliamuru kuwashwa kwa vituo vya habari hivyo vitatu na serikali na kuiagiza serikali kutoingilia utendaji kazi wa vituo hivyo hadi kesi hiyo itakaposikilizwa kikamilifu.
chanzo:bbcswahili

No comments:

Post a Comment