MAHAKAMA YATOA SIKU 14 KESI YA UHUJUMU UCHUMI -MAAFISA WIZARA MADINI - TANZA MEDIA ONLINE

Tuesday, 27 February 2018

MAHAKAMA YATOA SIKU 14 KESI YA UHUJUMU UCHUMI -MAAFISA WIZARA MADINI


Leo February 27, 2018 Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeutaka upande wa mashtaka ndani ya siku 14 kueleza ni lini Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP) ataendelea na kesi ya Uhujumu Uchumi wa kuisababishia Serikali hasara ya Bilioni 2.4 inayomkabili Mkurugenzi wa Tathmini ya Madini nchini,  Archard Kalugendo na mwenzake.
Hayo yamesemwa na Hakimu Mkazi Mkuu, Respicius Mwijage baada ya wakili wa serikali Elizabeth Nkule kudai kuwa upelelezi wa kesi hiyo umekamilika, jalada la kesi lipo kwa DPP, hivyo anaomba kesi ipangiwe tarehe nyingine.
Hata hivyo, wakili wa utetezi Ludovic Nickson amedai kuwa jamuhuri wanaleta hoja hiyo zaidi ya mara tatu katika tarehe tofauti November 9, 2017, January 3, 2018 na January 17,2018.
Tunachosubiri ni upelelezi kukamilika na kesi kusikilizwa kati ya Kisutu au Mahakama kuu na tunataka kufahamu DPP anachukua muda gani kukamilisha upelelezi” -Wakili Ludovic
Amedai kama DPP bado ana kazi nyingi awaruhusu watuhumiwa kuomba dhamana wakati anaendelea na shughuli zake ili watuhumiwa wawe nje.
Mshtakiwa mwingine katika kesi hiyo ni  Mthamini wa Madini ya Almasi wa Serikali, Edward Rweyemamu na wote wanakabiliwa na shtaka  hilo.
Baada ya kuelezwa hayo, Hakimu Mwijage ameahirishwa kesi hiyo hadi March 12, 2018kwa ajili ya kutajwa
Inadaiwa kuwa kati ya August 25 na 31, 2017  katika maeneo mbalimbali kati ya Dar es Salaam na Shinyanga, washtakiwa kwa pamoja na kwa vitendo vyao wakiwa wathamini  wa Madini waliisababishia hasara Serikali kiasi hicho cha fedh
a

No comments:

Post a Comment