CHAMA cha Demkorasia na Maendeleo (Chadema) kimekusudia kukata rufaa ya kupinga hukumu iliyotolewa leo dhidi ya Mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi ‘Sugu’ na Katibu wa Chadema Kanda ya Nyanda za Juu Kusini, Emmanuel Masonga, waliyohukumiwa kifungo cha miezi mitano jela baada ya kutiwa hatiani kwa kosa la kutoa maneno ya kumfedhehesha Rais Magufuli.
Makamu Mwenyekiti wa Chadema Prof. Abdalla Safari amesema chama hicho kinapinga hukumu hiyo kwa kuwa ina mapungufu ya kisheria, pia amesema mawakili wameshaanza kushughulikia rufaa na suala la dhamana endapo watakubaliwa.
Taarifa iliyotolewa na Kada wa Chadema, Godlisten Joseph Malisa kupitia Instagram imesema“Mawakili wanaomtetea Sugu na Masonga wakiongozwa na Boniphace Mwabukusi wapo mahakamani kuandaa maombi ya dhamana ya wateja wao na kukata rufaa. Wamepewa muda wa kuandaa rufaa hiyo na kuiwasilisha leo kabla ya muda wa mahakama kuisha.”
No comments:
Post a Comment