Serikali hiyo imejitosa kumshawishi Rais Kabila aachie ngazi ili kuheshimu Katiba na zaidi sana, kukubaliana na matakwa ya wananchi wengi
Taarifa ya serikali hiyo imeeleza kuwepo kwa kila dalili kuwa Congo itatumbukia katika machafuko na vita vitakavyosababisha vifo vya raia wasiokuwa na hatia
Kabila alichukua urais mwaka 2001 baada ya mauaji ya baba yake na alitarajiwa kuachia madaraka mwaka 2016 baada ya kipindi cha miaka miwili ya uongozi kuisha
Hata hivyo, amekuwa akitoa changamoto mbalimbali ambazo zimezuia Shirika la Uchaguzi kufanya uchaguzi wa rais mwingine
Tarehe mpya ya Desemba 23, 2018 imewekwa kwa ajili ya Uchaguzi lakini wafuasi wa upinzani wanataka Kabila kutangaza kuwa hatatafuta kubadili Katiba ya nchi ili kumfanya aendelee kukaa madarakan
No comments:
Post a Comment